Yesu Yuaja na Utukufu Wake
Yesu yuaja, na utukufu wake,
Kuwapokea waaminifu wake;
Labda atakuja hapa asubuhi
Wakati wa pambazuko.
Chorus
Bwana Yesu, lini, lini,
Tutakapoimba?
Kristo Yupo, Aleluya!
Aleluya Amin, Aleluya Amin!
Yesu atakuja labda adhuhuri,
Labda ataonekana magharibi;
Ama katika usiku wa manane,
Pamoja na utukufu.
Watu wakimwimbia Yesu, Hozana,
Pamoja na malaika wake Bwana;
Kwa neema yake atatupokea,
Yesu atakaporudi.
Furaha nyingi! tutaishi mbinguni,
Hakuna ugonjwa wala kufariki;
Hatutakuwa na hofu duniani,
Yesu atakaporudi.
Home