Nitwae Hivi Nilivyo
Nitwae hivi nilivyo,
Umemwaga damu yako,
Nawe ulivyoniita,
Bwana Yesu, naja.
Hivi nilivyo; si langu
Kujiosha roho yangu;
Nisamehe dhambi zangu,
Bwana Yesu naja.
Hivi nilivyo; sioni
Kamwe furaha moyoni;
Daima ni mashakani,
Bwana Yesu, naja.
Hivi nilivyo kipofu,
Maskini na mpungufu;
Wewe u mtimilifu,
Bwana Yesu, naja.
Nawe hivi utanitwaa;
Nisisubutu kukawa,
Na wewe hutanikataa
Bwana Yesu, naja.
Hivi nilivyo; mapenzi
Yamenipa njia wazi;
Hali na mali sisazi,
Bwana Yesu, naja.
Home