Nikilemewa na Mizigo Mingi

Nikilemewa na mizigo mingi,
Nikitembea bila tumaini;
Mwokozi wangu ameniahidi,
Niambie ahadi zake tena.

chorus
Niiambie ahadi tena,
Mara kwa mara ahadi tena;
Na nitafurahi, hapana huzuni,
Niambie ahadi zake tena.

Nikizungukwa na hatari nyingi,
Na nikishikwa na hofu rnoyoni;
"Sitakuacha," asema Mwokozi,
Niambie ahadi zake tena.

Na nikiingia mbinguni kwake,
Kupumzika salamani milele;
Ahadi zake tamu, zikumbukwe,
Niambie ahadi zake tena.

Home





Next song