Nadumu kwa Ahadi

Nadumu kwa ahadi zake Mfalme,
Yesu asifiwe kwa siku zote;
Nitamwimbia sana, Atukuzwe,
Kudumu kwa ahadi zake.

Chorus
Dumu, Dumu,
Nadumu kwa ahadi za
Bwana wangu;
Dumu, Dumu,
Nadumu kwa ahadi za
Mungu.

Nadumu kwa ahadi, sina shaka,
Ahadi zisizokosa kabisa;
Kwa Neno lake Mungu, nitashinda;
Kudumu kwa ahadi zake.

Nadumu kwa ahadi, nafahamu
Nina utakaso mkamilifu;
Kudumu kwa uhuru wake Yesu,
Kudumu kwa ahadi zake.

Nadumu kwa ahadi zake Kristo,
Kwa milele nimefungwa na pendo;
Nitashinda kwa upanga wa Roho,
Kudumu kwa ahadi zake.

Nadumu kwa ahadi, sitakosa,
Sauti ya Roho nitasikia;
Katika Mwokozi nimepumzika,
Kudumu kwa ahadi zake.

Home





Next song