Damu Imebubujika

Damu imebubujika,
Ni ya Imanweli,
Wakioga wenye taka
Husafiwa kweli (3)

Ilimpa kushukuru
Mwivi mautini;
Nami nisiye udhuru,
Yanisafi ndani. (3)

Kondoo wa kuuawa,
Damu wa nguvu,
Wako wote kuokoa
Kwa utimilivu. (3)

Bwana, tangu damu yako
Kunisafi kale,
Nimeimba sifa zako;
Taimba milele. (3)

Nikifa tazidi kwimba
Sifa za wokovu,
Ulimi ujaponyamaa
Vumbini mwa ufu. (3)

Bwana, umenikirimu
Nisiyestahili
Kwa damu- yako, sehemu
Ya mali ya kweli. (3)

Nikikubali kukwimbia,
Mbinguni milele
Mungu nitalisifia
Jina lako pweke. (3)

Home





Next song