Nimehitaji Mwokozi

Nimehitaji Mwokozi,
Awe nami daima;
Nataka mikono yake
Kunizunguka sana.

Chorus
Hofu rohoni sina,
Aniongoze tena;
Sitanung'unika tena,
Nimfuate daima.

Nimehitaji Mwokozi,
Sina imani nyingi;
Atanifufusha moyo,
Wengine hawawezi.

Nimehitaji Mwokozi,
Mwendoni mwa maisha;
Katika mateso mengi,
Tena katika vita.

Nimehitaji Mwokozi,
Kiongozi njiani;
Kwa jicho aniongoze
Nifike mbinguni.

Home





Next song