Tangu Siku Hiyo
Tangu siku hiyo aliponijia,
Akae moyoni mwangu;
Sina giza tena, ila mwanga pia
Kwa Yesu Mwokozi wangu.
Chorus
Amani moyoni mwangu,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu;
Sina shaka kamwe
Kwa sababu Yeye
Yu nami moyoni mwangu.
Sina haja tena ya kutangatanga,
Ndiye Kiongozi wangu;
Dhambi zangu zote zimeondolewa
Na Yesu, Mwanawe Mungu.
Matumaini yangu ni ya hakika,
Katika Mwokozi wangu;
Hofu zangu na hamu zimeondoka,
Kwa kuwa ninaye Yesu.
Siogopi tena nikiitwa kufa,
Yu nami, daima, Yesu;
Mlango wa Mbinguni ni Yeye pia,
"Tapita humo kwa damu."
Nitaketi na Yeye huko milele,
Nisifu Mwokozi wangu;
Nina raha moyoni majira yote
Kwa Yesu, Mwanawe Mungu.
Home