Ahadi ya Bwana
Ahadi ya Bwana twaingojea,
Kutoka mbingu itatujalia;
Ewa imani yetu twaipokea,
Kungoja orofani.
Chorus
Uwezo! Uwezo!
Hutupa ushindi
Na usafi ndani;
Uwezo! Uwezo!
Uwezo wa Pentekoste.
Kwake Bwana Yesu tutamtolea,
Kutoka dhambi atatufungua;
Pumzi ya uzima tutaipata,
Kungoja orofani.
Twatamani kuendelea mbele,
Kumngojea Bwana tupate tele;
Moto wa Mbingu na ututakase,
Kungoja orofani.
Home