Tutume, Tutume
Tutume, tutume, ya Mungu tutume;
Twandame njia yake wetu mfalme;
Kila neno tufanye kwa nguvu zetu
Ambalo yaliona mikono yetu.
Chorus
Kwa bidii, kwa bidii;
Kwa bidii, kwa bidii;
Na twombe tukeshe
Tutume hata aje Bwana.
Tutume, tutume, wa njaa walishwe,
Maji ya uzima wa kiu wanyweshwe;
Msalaba, beramu yetu ing'are,
Twahubiri wote neema bure.
Tutume, tutume, sote na tutume,
Ya giza na uwongo enzi ikome;
Ikue ya Bwana; sana na tung'are
Tushukuru kwa neema kuwa bure.
Tutume, tutume, kwa nguvu za Bwana;
Mwisho vao na taji vyapatikana,
Watakatifu kama jua wang'are,
Twimbe sote kwa neema kuwa bure.
Home