Mkuu Akamjia Yesu Usiku

Mkuu alinijia Yesu usiku,
Kwa kumwuliza njia ya wokovu;
Kwa udhahiri akamjibu Bwana,
"Uzaliwe tena."

Chorus
"Uzaliwe tena,
Uzaliwe tena;
Amini, Amini, nakuambia,
Uzaliwe tena."

Sikilizeni, Enyi wanadamu,
Na lishikeni Neno lake tamu;
Jinsi Yesu kwako alivyonena,
'UzalIwe tena."

Enyi mtakaoingia raha,
Kuimba na waliokombolewa;
Ukipate kipawa cha uzima,
"Uzaliwe tena."

Mpendwa wako aliye mbinguni,
Atakukaribisha miangoni;
Uyasikie maneno ya Bwana,
"Uzaliwe tena."

Home