Umealikwa
Umealikwa, uje sasa,
Karamu imeandikwa;
Uje sasa uliyechoka,
Na utabarikiwa.
Chorus
Itika mwaliko,
Kwa awaye yote;
Mungu na asifiwe,
Kwa wokovu wake.
Umealikwa, uje sasa,
Uje utakaribishwa;
Na utaheshimiwa sana,
Utaketi na Bwana.
Umealikwa, uje sasa
Uje anakungojea;
Usikawie, uje leo,
Labda utachelewa.
Umealikwa uje sasa,
Acha masumbuko yote;
Uje ule pendo la Mungu
Tapata utulivu.
Home