Enda Nasi

Tunaomba uwepo wako uende nasi
Ewe Bwana wa majeshi utusikie
Kama hauendi nasi, hatutaki kutoka hapa
Hatuwezi pekee yetu, enda nasi
Tu watu wa shingo ngumu tusamehe
Hatufai mbele zako, turehemu
Tusafishe ee Baba, tuonyeshe uso wako
Twahitaji neema yako, enda nasi

Tutavua mapambo yetu
Na vitu vyote vya dhamani kwetu
Mioyo yetu twaleta mbele zako
Tutakase na utembe nasi

Tunaomba utuonyeshe njia zako
Kwa maana umetuita kwa jina
Twalilia Ee Bwana, utukufu na uso wako
Bila wewe tutashindwa, enda nasi

Tutavua mapambo yetu
Na vitu vyote vya dhamani kwetu
Mioyo yetu twaleta mbele zako
Tutakase na utembe nasi

Home





Next song