Kutoka Dhambini

Kutoka dhambini mpaka rnbingu,
Nimeshikwa na pendo la Mungu;
Kwa vifungoni nimeondoka,
Na Yesu hunishika.

chorus
Yesu hunishika,
Yesu hunishika;
Kutoka gizani mpaka mwanga,
Na Yesu hunishika.

Kutoka taabu mpaka raha,
Nimefika nchi ya baraka;
Kwa fahari yake nitakaa,
Na Yesu hunishika.

Kwa kujitoa nitamwabudu,
Kwa pendo lake nitamshukuru;
Kwa milele naye nitakaa,
Na Yesu hunishika.

Home





Next song