Zamani Watoto Waliletwa

Zamani watoto waliletwa kwa Yesu,
Wanafunzi walitaka kuwafukuza,
Kabla hawajaondoka akawaita haraka,
Watoto wadogo na waje kwangu."

Nitawakubali, nami nitawalea,
Ni Mchunga wao hawa, msiwafukuze;
Wakinipenda mioyoni, na waje kwangu
mbinguni,
Watoto wadogo na waje kwangu."

Ndiye Bwana rnwema, huwaita watoto,
Lakini wako wengi wasiomjua,
Hawajui Chuo chake, wala lile neno lake,
Watoto wadogo na waje kwangu."

Na kila kabila ya watu duniani,
Waje kwa Yesu, watupe sanamu zao;
Ewe Mungu wa mapenzi, wapeleke wakufunzi,
Wakafunze wote, wafike kwako.

Home





Next song