Yesu, Nikikukumbuka

Yesu, nikikukumbuka
Huona tamu moyo,
Itazidi nikikwona
Uso ukaapo.

Hakuna kamwe tamko
Lenye kusemeka,
Tamu kama Jina hilo,
Wala kuwazika.

Jinsi ilivyo, hakuna,
Tangu kale kitu
Cha kuzidi lako Jina
Mwokozi wa watu.

Tumai ya watubuo,
Nyemi za wapole,
Wa kuomba, watafutao,
Wabariki wale.

Ulivyo kwa wakwonao
Havijulikani,
Pendo zako wajuao
Ndio wa pendoni.

Yesu huku U raha kuu,
U ujira kule:
Ni Wewe letu shangwe tu,
Milele, milele.

Home