Niimbie Mara Mara

Niimbie mara mara
Maneno ya uzima!
Nione zaidi tena
Neno la uzima.
Neno lenye uzuri!
Hufundisha habari.

Chorus
La ajabu! La ajabu!
Ndilo Neno lake Yesu!
La ajabu! La ajabu!
Neno lake Yesu!

Kristo Yu mwenye kutoa
Maneno ya uzima!
Mwenye dhambi kuokoka
Neno la uzima!
Tumeupata bure
Uzima wa milele!

Injili uitangaze,
Maneno ya uzima!
Amani wote wapate,
Neno la Uzima!
Yesu ndiye MWokozi!
Milele Kiongozi!

Home





Next song