Kwa Mji Wa Mwangaza
Kwa mji wa mwangaza
Hapana usiku;
Hautapita tena,
Hapana usiku.
chorus
Mungu atayafuta
Machozi na hasara;
Hapo miaka itakoma
Hapana usiku.
Jua halitakiwi
Hapana usiku;
Yesu ni nuru, kweli,
Hapana usiku.
Kwa mji wa mbinguni
Hapana usiku;
Milele furahini,
Hapana usiku.
Home