Kijito Cha Utakaso
Kijito cha utakaso
Ni damu ya Yesu,
Bwana anao uwezo
Kunipa wokovu.
chorus
Kijito cha utakaso,
Nizame kuoshwa humo;
Namsifu Bwana kwa hiyo,
Nimepata utakaso.
Viumbe vipya naona,
Damu ina nguvu;
Imeharibu uovu,
Uliodhulumu.
Naondoka kutembea
Nuruni mwa mbingu,
Na moyo safi kabisa
Kumpendeza Mungu.
Ni neema ya ajabu,
Kupakwa na damu;
Na Bwana Yesu kumjua,
Yesu wa Msalaba.
Home