Mtazame Huyo
Mtazame Huyo!
Aliyeangikwa juu
Hivi sasa upate ishi.
Mwenye-dhambi dhaifu,
mtazame tu
Wala usifanye tashwishi.
Chorus
Tazama! Tazama! uishi!
Mtazame Huyo aliyeangikwa Juu
Hivi sasa upate ishi.
Kama siye Kondoo
Mwondoa-dhambi,
Na makosa yako ya mumu!
Kama deni zetu zote hakulipa
Mbona imemwagika damu?
Si kutubu na sala ikomboayo
Ila damu ndiyo salama;
Na aliyemwaga aweza, sasa,
Dhambi zako kukufutia.
Usiwe na shaka,
Mungu amesema,
Hakuna alilolisaza;
Hapo alipokuja alitimiza,
Kazi zote alizoanza.
Basi twae uzima kwa kufurahi
Upokee kwa Bwana, sasa,
Ujijue hakika kwake kuishi
Yesu, aishiye kabisa.
Home