Imbeni juu ya Pendo

Imbeni juu ya pendo La Yesu,
Na imbeni juu ya rehema;
Makao atufanyia,
Tumepewa neema.

chorus
Tuendapo mbinguni,
Itakuwa siku ya salama;
Tumwonapo Yesu,
Tutamshangilia Bwana.

Tukisafiri njiani mwetu,
Tutazikuta shaka nyingi;
Bali tukifika mwisho,
Hapo tutafurahi.

Tuwe waamini na wanyofu,
Na tumhudumu kila siku;
Tutamwona kwake mbingu,
Hiyo ni utukufu.

Twende mbele kupata zawadi,
Ni karibu kumwona Yesu;
Milango itafunguka
Tuingiapo mbingu.

Home





Next song