Msalabani Pa Mwokozi
Msalabani pa Mwokozi
Hapo niliomba upozi,
Akaniokoa Mpenzi,
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Akaniokoa Mpenzi, Mwana wa Mungu.
Chini ya mti msumbufu
Niliomba utakatifu,
Alinikomboa kwa damu,
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Alinikomboa kwa damu,
Mwana wa Mungu.
Aliniokoa dhambini,
Ikawa kunikaa ndani,
Aliponifia mtini, -
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Aliponifia mtini, Mwana wa, Mungu
Damu ya Yesu ya thamani
Huniokoa makosani,
Huniendesha wokovuni
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu
Huniendesha wokovuni, Mwana wa Mungu.
Hicho kijito cha gharama
Leo jivike kwa kuzama,
Kwake uuone uzima,
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Kwake uuone uzima, Mwana wa Mungu.
Home