Uzima na Pendo Langu
Uzima na pendo langu
Nakupea Mungu wangu,
Niwe mwaminifu kwako,
Ee Mwokozi wangu.
Chorus
Kwako Bwana, nikiishi
Nitapata kufurahi,
Kwa kuwa umejitoa,
Ee Mwokozi wangu.
Naamini kwako Bwana,
Ili nipate uzima;
Sasa nakutegemea,
Ee Mwokozi wangu.
Kwa Kalvari ulikufa
Ili nipate kupona;
Sasa nakujitolea,
Ee Mwokozi wangu.
Home