Namwandama Bwana
Namwandama Bwana
kwa alilonena,
Njia yangu huning'azia;
Nikimridhisha atanidumisha
Taamini nitii pia.
Chorus
Amini utii,
Njia pweke ni hii
Ya furaha kwa Yesu:
Amini ukatii.
Giza sina kwangu
wala hata wingu
Yeye mara huviondoa;
Oga, wasiwasi, sononeko, basi;
Huamini nitii pia.
Masumbuko yote,
sikitiko lote;
Kwa mapenzi hunilipia;
Baa, dhara, dhiki,
vivyo hubariki.
Taamini nitii pia.
Mimi sitajua
raha sawasawa
Ila yote Yesu kumpa;
Napata fadhili
na radhi kamili,
Taamini nitii, pia.
Nitamfurahi na kumtumai,
Majumbani na njia-njia;
Agizo natenda;
nikitumwa hwenda,,
Huamini nitii pia.
Home