Baba Narudi

Nilipotea katika dhambi
Nikawa mtumwa wa shetani
Nimechoka na mzigo wa dhambi
Baba narudi

Nimekukimbilia wewe Mungu wangu
Nisiaibike milele
Kwa haki yako baba uniponye
Unitegee sikio lako

Nimetanga mbali na urithi wangu
Neno lililofunuliwa
Nipokee jinsi nilivyo
Baba narudi

Mikononi msalimie wewe Baba
Naiweka roho yangu
Najua siku zangu ziko mikononi mwako
Baba narudi

Home





Next song