Bwana, U Sehemu Yangu
Bwana, U sehemu yangu,
Rafiki yangu, Wewe;
Katika safari yangu
Tatembea na Wewe
Pamoja na Wewe,
Pamoja na Wewe,
Katika safari yangu
Tatembea na Wewe.
Mali hapa sikutaka
Ili niheshimiwe,
Na yanikute mashaka
Sawasawa na Wewe.
Pamoja na Wewe,
Pamoja na Wewe,
Heri nikute mashaka
Sawasawa na Wewe.
Niongoze safarini,
Mbele unichukue,
Mlangoni mwa mbinguni
Niingie na Wewe.
Pamoja na Wewe,
Pamoja na Wewe,
Mlangoni mwa mbinguni
Niingie na Wewe.
Home