Chini ya Mizigo ya Dhambi

Chini ya mizigo ya dhambi,
Watu wengi walemewa;
Bali waweza kufurahi,
Wakipokea uzima.

Chorus
Uzima, uzima,
Yesa ndiye Mtoaji;
Uzima daima,
Asifiwe Mwokozi.

Mwenye mizigo usishike
Huzuni zilizo tele;
Ufungue moyo ujazwe
Na uzima wa milele.

Kama mto ulivyotoka
Mlima, kutuliza bonde;
Ndivyo kutoka Msalaba,
Uko uzima wa tele.

Nehi kavu igarikishwe,
Na tupate ufufuo;
Tusiogope, tutakaswe,
Kutangaza ufufuo.

Home