Siku ya Mbingu

Siku ya mbingu kujawa na sifa,
Dhambi zilizidi duniani;
Yesu akaja azaliwe mtu,
Awe na watu ulimwenguni.

Chorus
Alinipenda, alinifia,
Ameondoa na dhambi zangu;
Alifufuka nipewe haki,
Yuaja tena Mwokozi wangu.

Na siku moja walikwenda naye
Wakamkaza Msalabani;
Aliumia, aliaibishwa,
Ili atuokoe dhambini.

Siku hiyo wakamIaza chini
Kaburini, alipumzika;
Matumaini yetu wenye dharnbi,
Ni Mwokozi, kwake twaokoka.

Kaburi likashindwa kumshika;
Jiwe likatoka mlangoni,
Alifufuka, kwa kushinda kwake,
Naye yuko nillele rnbinguni.

Siku moja atatujia tena;
Utukufu wake tutaona;
Atawaleta na wapenzi wetu;
Mwokozi wangu, tutaonana.

Home





Next song