Maombi Yangu

Wakati wa matatizo najiuliza maswali
Kweli bwana Mungu yuko karibu na mimi
Shida zanifunga macho
Nikawa sioni mbele
Kweli dunia hii ina matatizo

Sikia maombi yangu bwana, ninakuomba
Nipe Imani
Shida nyingi zinanisonga na sina uwezo
Nishindie bwana daima

Na wakati wa furaha naanza kufikiria
Wema na uzuri wako na vile unanipenda
Siyapendi matatizo lakini nafurahia
Vile nguvu zako zaniwezesha kushinda

Ninawaombea wale ambao Ni wadhaifu
Waongezee amani
Wapate kuwa na raha
Wape Imani wapate kuku tumaini wewe
Ndipo wapate kujua nguvu zako bwana.

Home





Next song