Deni Yangu ya Dhambi
Deni yangu ya dhambi,
Yesu amelipa;
Kwake Msalabani
Nilipewa uzima.
Chorus
Deni ya dhambi,
Msalabani;
Ilimalizikia
Ni huru kabisa.
Bwana Yesu asema,
"Mwanangu dhaifu,
Uwezo na ushindi,
Hupatikana kwangu."
Bwana, kweli naona,
Nguvu zako pekee;
Huondoa ukoma,
Niwe kipya kiumbe.
Sina wema moyoni,
Nidai neema;
Nakubali kabisa,
Kwa damu kusafiwa.
Hata huko Mbinguni,
Miguuni pake;
"Yesu alinifia,"
Nitaimba milele.
Home