Neno Lake Yesu
Neno lake Yesu, na ahadi
Zimepita jumbe zote duniani,
Kristo Mtakatifu, hana dhambi,
Yeye ni Kielelezo kwangu mimi.
Chorus
Ninapoongozwa,
Na Yesu Bwana;
Ninapoongozwa,
Kweli, nitamwandama.
Pendo lake Yesu, naliona,
Lashinda pendo zo zote za dunia;
Yesu Mwaminifu, huokoa,
Yeye ni Kielelezo kwangu sasa.
Yesu anasema, "Uje kwangu,
Ulemewaye upate raha yangu;"
Amini ahadi zake Bwana,
Mtegemee Mwokozi kwa salama.
Home