Mungu Alipenda Ulimwengu

Mungu alipenda ulimwengu,
Akamtoa Mwana wake;
Kila mtu amwaminiye,
Na uzima apate.

Chorus
Ni kweli ndiyo kweli,
Ahadi zake zi kweli;
Neno lake Mungu ladumu,
Ahadi zake zi kweli.

Nikawa mwana asiye mwema,
Kwa dhambi nikawa mtumwa;
Hata nikapata baraka
Iliyonipendeza.

Neno la Bwana nikakubali
Aliposema na mimi;
Ahadi nikazisadiki,
Nikatengwa na dhambi.

Ninao uzima wake Mungu,
Moyo wangu llmejazwa;
Na nitamsifu Bwana Yesu
Aliyenikomboa

Home