Mapenzi Yako Yafanyike

Mapenzi yako yafanyike,
Wewe Mfinyanzi, nami towe;
Unifinyange upendavyo,
Mimi tayari, naja kwako.

Mapenzi yako yafanyike,
Unihojie dhambi zote;
Unisafishe vya kimwili,
Niinamapo Msalabani.

Mapenzi yako yafanyike,
Mimi dhaifu, mimi mnyonge;
Uwezo wote, kwako kweli,
Sasa niponye, Ee Mwokozi.

Mapenzi yako yafanyike,
Natoa kwako vitu vyote:
Maisha, mali, moyo, mwili,
Vyote ni vyako, kweli, kweli.

Mapenzi yako yafanyike,
Mapenzi yangu yavunjike;
Ninakubali uwe Bwana,
Ni mali yako, twaa kabisa.

Mapenzi yako yafanyike,
Unitawale siku zote;
Sura ya Yesu umba kwangu,
Nijaze Roho naye nguvu.

Home





Next song