Siku kwa Siku, Bwana Nilinde

Siku kwa siku, Bwana nilinde,
Ilii nikuamini ko kote;
Gizani, mwangani, haidhuru,
Nitaujua wema wa Mungu.

chorus
Kuamini, kuamini,
Nipate nguvu ya kuamini;
Ijapokuwa taabu nyingi,
Nipate fadhili ya kuamini.

Nisiogope mambo ya kesho,
Nitapokea neema yako;
Yote ambayo yatanijia,
Nijue kwamba umenipenda.

Siku kwa siku nikuamini,
Nitakuona kwako mbinguni;
Nikiteswa humu duniani,
Hapo nitazidi kuamini.

Home





Next song