Ndiyo Dhamana

Ndiyo dhamana, Yesu wangu,
Hunipa furaha za Mbingu;
Mrithi wa wokovu wake,
Nimezawa kwa Roho yake.

Chorus
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu:
Habari njema, raha yangu
Yesu ndiye Mwokozi wangu

Kumsalimu moyo wangu,
Mara namwona raha yangu;
Aniletea malaika,
Wananilinda, taokoka.

Sina kinyume, nashukuru,
Mchana kutwa huja kwangu;
Usiku kucha kuna nuru,
Mwokozi wangu, ndimi huru.

Hali na mali, anitwaa!
Mara namwona anifaa;
Nami nangoja kwa subira
Akiniita, nije mara.

Home





Next song