Ni Wako Wewe, Nimekujua

Ni wako Wewe, nimekujua,
Na umeniambia;
Lakini Bwana, nataka kwako
Nizidi kusongea.

Chorus
Bwana vuta, vuta, nije nisongee,
Sana, kwako Mtini.
Bwana vuta, vuta, nije nisongee,
Pa damu ya thamani.

Niweke sasa nikatumike
Kwa nguvu za neema;
Uyapendayo nami nipende
Nizidi kukwandama.

Nina furaha tele kila saa
Nizungumzapo kwako,
Nikuombapo, nami napata,
Kujua nia yako.

Mapenzi yako hayapimiki,
Ila ng'ambo ya liko.
Anasa pia sitazijua,
Bila kufika kwako.

Home





Next song