Ebu Nieleze

Bwana niambie kile kilichokufanya
Ukaja huku wakati ule
Yote ya mbinguni huku yaona kitu
Ukaja ishi na watu wako

Bwana
Ebu nieleze kwa sauti ya upole
Akili zangu Bwana ni fupi
Rudi rudia kama vile kwa mtoto
Nisisahau hata kidogo

Walipokusulubisha msalabani
Hakuna aliyekusaidia
Ukafa kifo cha uchungu na aibu
Kwa dhambi zisizo kuwa zako

Zidi kunionyesha ubaya wa dhambi
Najua ndizo zilizokuuwa
Na ningekuwapo Bwana kutenda dhambi
Ebu nirudishe kwa fimbo yako

Bwana
Ebu nieleze kwa sauti ya upole
Akili zangu Bwana ni fupi
Rudi rudia kama vile kwa mtoto
Nisisahau neno lako

Bwana niambie kwa sauti ya upole
Akili zangu zikuelewe
Rudia rudia kama vile kwa mtoto
Nisisahau hata kidogo

Home





Next song