Nionapo Amani Kama Shwari

Nionapo amani kama shwari,
Au nionapo shida;
Kwa hail zote umenijulisha
Ni salama rohoni mwangu.

Chorus
Salama rohoni,
Ni salama rohoni mwangu.

Ingawa Shetani atanitesa,
Nitajipa moyo kwani
Kristo ameona unyonge wangu
Amekufa kwa roho yangu.

Dhambi zangu zote, wala si nusu,
Zimewekwa Msalabani;
Wala sichukui laana yake,
Ni salama rohoni mwangu.

Ee Bwana, himiza siku ya kuja,
Panda itakapolia;
Utakaposhuka sitaogopa,
Ni salama rohoni mwangu.

Home





Next song