Nimeifikia Nchi
Nimeifikia nchi,
Ya nafaka na asali;
Mwanga hung'ara daima,
Na usiku umekoma.
Chorus
Nchi nzuri, nchi nzuri,
Nasimama mlimani,
Naona nchi ya mbali
Iliyowekwa tayari;
Niitazamie pwani
Ya nchi yangu mbinguni.
Mwokozi wangu yu nami,
Twashirikiana kweli;
Aniongoza mkononi,
Nifike kwake mbinguni.
Nazisikia sauti
Za malaika mbinguni,
Wamwimbie Bwana sifa
Na wale waliookoka.
Home