Msikie Bwana

Msikie Bwana anawaita,
wenye kulemewa wasumbukao,
njoo kwake Yesu akupumzishe,
kila shida zote atachukua.

Uje leo(uje leo), akupumzishe,
nira yake Bwana, ni nyepesi mno.
Yeye mnyenyekevu, mpole kabisa,
mwepesi mzigo(mwepesi mzigo), Njoo kwake leo!

Umechoka sana,
rohoni mwako,
na mashaka mengi unayaona,
njoo kwake Yesu na shida zote
leo akuita akupimzishe.

Umepotea dhambini kabisa,
hukumu milele utaingia,
lakini Mchungaji, ndiye Mwokozi,
atakuokoa, ukija kwake.

Je majaribuni, wewe hushindi,
uje kwake Yesu, nguvu upewe,
anao uwezo kukushindisha,
Roho Mtakatifu akupumzishe.

Home





Next song