Msifuni, Yesu Ndiye Mkombozi

Msifuni Yesu ndiye Mkombozi;
Imbeni ya pendo zake kuu;
Sujuduni, malaika mlioko,
Jina lake liwe na sifa kuu.

Kama vile mchunga achungavyo
Vivyo sisi kutwa atuchunga.
Msifuni mlio wake watoto
Msifuni aliye Mchunga.

Msifuni, Yesu ndiye Mkombozi
Akateswa tupate ongoka;
Ndiye Mwamba, Dhamana ya kuokoka;
Sujudini kwake Muangikwa,

Yesu aliyeudhiwa na hamu
Kwa pendo za Baba yake Mungu.
Aliyefyolewa na kusulubiwa,
Msifuni ndilo letu fungu.

Msifuni, Yesu ndiye Mkombozi
Shindukeni, enyi malango, juu;
Bwana Yesu tangu milele Mwokozi,
Mvikeni taji, ni yake tu.

Atakuja kuitawala nchi,
Yesu, Mwombezi wetu wa Mungu.
Msifuni, ni Mfalme wa salama;
Ndiye kweli Mwana wake Mungu.

Home





Next song