Twendeni Askari
Twendeni askari, watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele, tumwandame juu
Ametangulia Bwana vitani, -
Twende mbele kwani ndiye amini.
Chorus
Twendeni askari
watu wa Mungu
Yesu yuko mbele,
tumwandame juu
Jeshi Ia Shetani, likisikia
Jina la Mwokozi, litakimbia,
Kelele za shangwe zivume nchi;
Ndugu, inueni zenu sauti.
Kweli kundi dogo, watu wa Mungu,
La mababa yetu ni letu fungu,
Hatutengwi nao, moja imani,
Tumaini moja, na moja dini.
Haya mbele watu nasi njiani,
Inueni mioyo, nanyi sifuni;
Heshima na sifa ni ya Mfalme,
Juu hata chini, sana zivume.
Home