Nitaimba juu ya Mkombozi
Nitaimba juu ya Mkombozi,
Jinsi alivyonipenda;
Aliteswa msalabani,
Nisipate kulaaniwa.
Chorus
Imbeni juu ya Mkombozi,
Kwa damu aniweka;
Nafidiwa msalabani
Deni zangu zafutwa.
Nitanena habari njema,
Jinsi nilivyookoka;
Kwa upendo na neema,
Anipatia fidia.
Nltamsifu Mkombozi wangu,
Jinsi atoavyo ushindi:
Kwa uwezo namshangilia;
Juu ya dhambi na mauti.
Nitamsifu Mkombozi wangu
Jinsi alivyonipenda;
Amenitolea uzima,
Nikae kwake daima.
Home
Next song