Mbele Yake Mwokozi
Mbele yake mwokozi wangu,
Je nisimame maskini?
sina cha kumtumikia,
cha kumpa sinacho.
Nisimame mbele ya Mungu,
Sina kitu cha kumpa,
Bila hata na tunda moja,
Je nisimame hivyo?
Siku nyingi nilizitupa,
Zingerudi siku zile,
Ningempa Mwokozi wangu,
Ningemtumikia.
Ndugu yangu amka leo,
Bwana bado akuita,
Kifoni hunayo nafasi,
Ya kumtumikia.
Utasimama mbele yake,
Huna kitu cha kumpa
Bila hata na tunda moja,
Je utakuwa hivyo?
Home
Next song