Baba Yangu Ana Mali Nyingi
Baba yangu ana mali nyingi,
Hushika hazina zote mkononi;
Fedha zote na mawe thamani,
Na dhahabu zote ulimwenguni.
chorus
Ni mwana wa Mfalme,
Mwana wa Mfalme;
Pamoja na Yesu,
Ni mwana wa Mfalme.
Mwana wa Baba, Mwokozi wangu,
Alitembea humu ulimwengu;
Bali anatuombea sasa,
Ili tuwe watu wake kabisa.
Nilitupwa mbali duniani,
Nikakubali kuwa mwenye dhambi;
Bali sasa nimeokolewa,
Kweli, jina langu limeandikwa.
Hema au nyumba, sioni shaka,
Makao mazuri nitayapata;
Nikihamishwa na watu wangu,
Nitafurahi na Mwokozi wangu.
Home