Yesu Bwana Wangu Anipenda

Yesu Bwana wangu anipenda,
Nguvu zote hazitatutenga;
Akatoa uzima wake,
Niwe mali yake.

chorus
Yesu ni Bwana wangu,
Mimi mali yake;
Si kwa muda wa miaka tu,
Bali kwa milele.

Nilipotea mbali dharnbini,
Yesu akaja toka mbinguni;
Akanivuta na pendo lake,
Niwe mali yake.

Furaha tele, nimeokoka,
Kutoka dhambi nimefunguka;
Akaniponya kwa damu yake,
Niwe mali yake.

Home