Waponyeni Watu Wamo Kifoni
Waponyeni watu wamo kifoni,
Watoeni walio shimoni;
Na aangukaye mumzuie;
Ya Bwana Yesu wahubirini.
Chorus
Walio kifoni waokoeni,
Mwokozi yuko, wahubirini.
Wajapokawia anangojea,
Awasubiri waje tobani;
Msiwadharau, muwaonyeni;
Huwasamehe; wakiamini
Mioyoni mwa ndani yule Shetani
Ameyaseta mawazo yao;
Lakini kwa Bwana huwa mazima,
Tukiwavuta kwa pole hao.
Kawaokoeni waje njiani;
Mutimize mapenzi ya Bwana;
Na kwa nguvu zake warudi kwake,
Kwa subira waonyeni sana.
Home