Sauti ya Mchunga Wetu

Sauti ya Mchunga wetu,
Naisikia kwa mwitu;
Anaita kondoo zake,
Waliotoroka kwake.

chorus
Walete, Walete,
Kutoka dhambini walete,
Walete, walete,
Na walete kwake Yesu.

Nani amsaidiaye
Yesu, wakosa apate?
Nani atakayeleta
Wale waliopotea?

Sauti zao nyikani,
Hata kutoka mlimani;
Tumesihiwa na Bwana
Kuwaleta na salama.

Home





Next song