Fedha Wala Dhahabu

Fedha wala dhahabu hazitosheki,
Kuninunulia wokovu wangu;
Damu ya Msalaba ndiyo ni msingi,
Kifo cha Mwokozi kimetosheka.

chorus
Nakombolewa, si kwa fedha,
Wala si kwa dhahabu;
Bei aliyoninunulia
Ni damu yake Yesu.

Fedha wala dhahabu hazitosheki,
Amri za Mungu zilinikataza;
Damu ya Msalaba ndiyo ni msingi,
Kifo cha Mwokozi hunituliza.

Fedha wala dhahabu hazitosheki,
Kuinunua njia ya uzima;
Damu ya Msalaba ndiyo ni msingi,
Kifo cha Mwokozi huleta raha.

Home





Next song