Yesu Mfalme Mwokozi Wangu

Yesu Mfalme, Mwokozi wangu,
Maisha yangu nimekupa;
Nafurahi kwa wokovu wangu,
Damu yako hunifungua.

Mwokozi wangu, Mwokozi wangu,
Ndiwe wa thamani na pendo;
Mwokozi wangu, Mwokozi wangu,
Nimejaa na sifa zako.

Kufunguliwa! Habari Njema!
Madoa yote yamefutwa;
Yesu akaja akae kwangu,
Kwa pendo lake nimewaka.

Yesu Bwana, nimekusujudu,
Hazina zangu ziwe zako;
Unifundishe nikutukuze,
Hata milele niwe wake.

Nifikapo mle mbinguni,
Nitaona uzuri wako;
Nitafurahi hata milele,
Nitakuwa na mfano wake.

Home





Next song