Panda Asubuhi
Panda asubuhi mbegu ya fadhili,
Panda adhuhuri, tena jioni;
Tutaingojea siku ya mavuno,
Tutafurahi kuleta mavuno.
Chorus
Leta mavuno, leta mavuno,
Tutafurahi kuleta mavuno;
Leta mavuno, leta mavuno,
Tutafurahi kuleta mavuno.
Na panda mwangani, tena kivulini,
Usiwe na hofu kwa baridi mkuu;
Na mwisho wa kazi kuvuna mavuno,
Tutafurahi kuleta mavuno.
Mvunieni Bwana kwa machozi mengi,
Ijapo twaona taabu nyingi;
Mwisho wa kilio tutakaribishwa,
Tutafurahi kuleta mavuno.
Home